Saturday, April 20, 2013

Maisha yalokua yasiyo na muelekeo










Mpango mzima ulitokea Aprili 13, mwaka huu katika Ufukwe wa Belinda, jijini Dar wakati mwanadafada huyo alipokuwa amealikwa katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa chuo hicho.
Kutokana na kivazi hicho alichokivaa na mvuto alionao staa huyo, baadhi ya madenti wakware walionekana wakipoteza usikivu wa hotuba ya mgeni rasmi na kubaki kumtazama.
“Mh! Rose ni mzuri jamani uongo dhambi, nilikuwa nikimuona katika runinga leo nimemuona live daaah!” alisikika denti mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Monday, April 1, 2013

SHILOLE ABANWA KUHUSU KUTONGOZA VIJANA WADOGO......!!!!

Wiki iliyopita katika safu hii tulimtambulisha kwenu msanii wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, kama kawaida maswali mengi yaliulizwa kama ifuatavyo: KWELI ALIOLEWA?
Eti ni kweli uliolewa na ulikuwa unaishi Keko? Khatibu, Dar, 0715456296.
SHILOLE: Kweli.
TABIA YA KUTONGOZA SERENGETI BOYS
Shilole acha kutongoza watoto wadogo halafu sauti ya kuimba huna, acha fani za watu. Sister Havinitishi, Dar, 0655196161.
SHILOLE: Mimi kwanza ni mdogo na siwatongozi watoto wadogo, kuhusu kuimba nitajifunza zaidi.
KUHUSU BABA WATOTO WAKE
Dada Shilole uko juu nakupa big up! Ningependa kufahamu hao watoto wako umezaa na baba mmoja au kila mtoto ana baba yake? Angel, Dar, 0714600415.
SHILOLE: Asante, watoto wangu kila mmoja ana baba yake.
HUYU AMEMZIMIA
Shilole naomba namba ya simu maana unanikosha wewe ni mzuri sana. Sangoti, Korogwe, 0654848387
SHILOLE: Asante, nitakutafuta.
KUHUSU MIDUME MCHARUKO MTAANI
Shilole wewe ni msanii mahiri kunako kiwanda cha filamu na muziki Bongo, je, unajiepusha vipi na midume inayokutokea kimapenzi? Salim Liundi, Dar, 0658110395.
SHILOLE: Asante, huwa najiepusha na midume kwa kujiheshimu na kujilinda hivyo siwapi nafasi.
UHUSIANO WAKE NA NGASSA
Shilole nataka kujua eti wewe na kiungo mahiri wa timu ya Simba Mrisho Ngassa mnatoka kimapenzi, mbona kuna tetesi za ajabu kitaani? Msomaji.
SHILOLE: Siyo kweli.
MZAZI MWENZAKE VIPI?
Umesema una watoto wawili, je vipi kuhusu mzazi mwenzio uko naye au ndiyo umemtema baada ya kupata umaarufu? Shariff Juma, Dar, 0713332349.
SHILOLE: Siko naye.
BIFU LAKE NA FLORA
Shilole hongera kwa kazi zako unajitahidi ila nataka kujua kwa nini hupatani na Flora Mvungi.  Silla, Dar, 0718764242.
SHILOLE: Asante, mimi sijagombana na mtu ila mti wenye matunda siku zote lazima upigwe mawe.
KUFICHA WATOTO WAKE
Zamani ulikuwa unaficha kama una watoto wawili mpaka mtu wako wa karibu alipotoa hiyo siri, kwa nini ulifanya hivyo? Cassian, 0655202202.
SHILOLE: Siyo kweli mbona watoto wangu wapo wazi!
KUHUSU MKOROGO
Big up! Shilole napenda muziki wako ushauri wangu kwako acha mkorogo unakuharibu. Tina, Mwanza, 0719747965.
SHILOLE: Siku hizi sipaki mkorogo, nimeacha.
SKENDO YA KUTOKA NA RAY
Dada Shilole unafanya kazi nzuri ila punguza skendo nasikia ulishawahi kutembea na Ray, je ni kweli? Charles Mallya, Mwanza, 0759022399.
SHILOLE: Asante, sijawahi kutembea na Ray.
BARNABA JE?
Shilole hivi ni kweli ulikuwa unatembea na Barnaba na kwa sasa mpenzi wako ni nani? Musa Mbughi, Sumbawanga, 0764021259.
SHILOLE: Siwezi kusema chochote.
UKWELI KUHUSU KUBAKWA
Shilole najua mtoto wako wa kwanza umezaa na Makala wa Igunga Tabora na ulikuwa unaishi naye kwa Tatu Balozi, ilikuwaje ukasema mwanaume aliyekupa mimba ya kwanza alikubaka? Ibrahim Yusuph, Dar, 0719599195.
SHILOLE: Sipendi kurudi nyuma ila ni kweli alinibaka nikapata ujauzito.
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Dada nataka kujua historia yako kiufupi. Sultan, Dar, 0654324222.
SHILOLE: Nimezaliwa Igunga Tabora nikiwa mtoto wa mwisho, sanaa nilianza mwaka 2010.

Obama tembea kwa Miguu kutoka White House hadi Kanisa la St. John’s Episcopal kwa sherehe ya Pasaka Washington DC .....!!!!

Rais Barack Obama akitembea kwa miguu na Familia yake kutoka White House across Pennsylvania Ave.  hadi Lafayette Park. huku akiwa amemshikili mtoto wake wa pili Sasha mkono pamoja, Mkewe Michelle Obama  na binti yao mkubwa Malia kuelekea katika Kanisa la St. John’s Episcopal liliopo Washington, DC ambapo walihudhuria  katika Pasaka  Siku ya Jumapili Machi 31, 2013. ( Official White House Picha na Pete Souza)
Pastor at Obamas Easter Church Service: Captains of the Religious Right Want Blacks in the Back of the Bus, Women Back in the Kitchen
Rais Barack Obama na first lady Michelle Obama walipotembea kutoka White House na binti zao Sasha Obama, wa pili kutoka kushoto, na Malia Obama, kulia, wakitembea kwa miguu kupitia Lafayette Park kwenda  katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington. (AP)

Obama alipokua akitembea Mitaa ya Lafayette Park  hadi  St. John's Episcopal Church Siku ya Jumapili  , March 31, 2013, ndani ya Jiji la Washington. (Picha na Carolyn Kaster)
OBAMAEASTER1N_2_WEB
Obamas akitembea kupitia Lafayette Park kwenda Kanisasani  kwajili ya Pasaka.
OBAMAEASTER1N_4_WEB
Rais wa Marekani Barack Obama na familia yake walipo maliza ibada katika Kanisa la St. John’s Episcopal kwa ajili ya Pasaka Siku Jumapili, Machi 31, 2013, Mjini Washington.  (Picha na YURI GRIPAS/REUTERS)

TIMU NNE ZITAINGIA KATIKA KIPINDI CHA TATU KUCHUANA VIKALI WIKI HII, NI KATIKA SHINDANO LA GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ MSIMU WA TATU (3)

Episode 3 team- bloggersTimu nne zitakazochuana katika kipindi cha tatu cha Guinness Football Challenge wiki hii. Kuanzia kushoto ni timu kutoka Kenya(wamevaa nyekundu), Tanzania –bluu, Uganda- kijani na nyeusi ni timu kutoka Kenya. TamashaMeneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi(kulia) na mtangazaji wa kipindi cha Tamasha la michezo Amry Masare wakijadili na kufanya uchambuzi wa kipindi cha kwanza na pili cha Guinness Football Challenge jana katika kipindi cha Tamasha la michezo kinachorushwa na televisheni ya ITV.
………………………………………………………………
Jumatano iliyopita  kupitia televisheni  za ITV na Clouds TV mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalituonesha ni kwanini ushirikiano ni muhimu kwa  washiriki kuonyesha ujuzi wao. Francis Ngigi and Kepha Kimani kutoka Kenya walifanikiwa kuingia hatua ya mwisho  na kujipatia fedha za kimarekani  dola 3,000 shukrani kwa vipaji vyao na ushirikiano mzuri.

 Francis na Kepha wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.

 GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .

 Katika Episodi ya tatu ya mashindano haya yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana siku ya Jumatano.
 Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali katika kipindi cha pili wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na televisheni za ITV na Clouds TV.

Timu ya bluu-Tanzania:
  • Mohamed Kobembe na Gullam Sosha wenye umri  wa miaka 23 kutoka Dar es Salaam watashirikiana kuona kama wataweza kushinda katika kipindi cha tatu cha GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE.Mohamed ndiye kichwa cha timu ni mwanafunzi  wa  shahada ya kwanza ya maswala ya kodi na Gullam ambaye ni mchezaji wa Ndanda FC, wana matarajio ya kufanya vizuri katika mashindano hayo. 
 Timu nyekundu-Kenya:
  • Kenneth Kamau mwalimu wa timu ya vijana(23) na Willis Ogutu(miaka 30) wote kutoka Nairobi watachezea Kenya.Keneth ataonesha maarifa yake ya soka  wakati Willis ataonesha uwezo wake wa kucheza mpira.
 Timu ya kijani-Uganda:
  • Kennedy Mwota(22) kutoka Naijanakumbi na Steven Nsubuga(25) kutoka Kampala.Kennedy ni mwanafunzi na Steven ni muhasibu.Kennedy ataonesha ujuzi wa soka  na steven kipaji chake cha kusakata kabumbu.
 Timu nyeusi-Kenya:
  • Wafanya biashara wa Nakuru,Stephen Kaguda,35 na Gideon Onyango,34, watavaa jezi meusi. Stephen ambaye ni mshabiki wa Barcelona FC atakuwa akijibu maswali wakati Gideon ambaye ni mshabiki wa Man Utd atachezea mpira.
 Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.   Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.  

 Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya, Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri, unatakiwa kufatilia  ukurasa huu ‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.

 GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.  Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku.
 Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya  Guiness wakati unaangalia kipindi hiki. 

 *Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane.  Tafadhali Kunywa kistarabu.

TAMASHA LA AIRTEL YATOSHA LATIKISA MKOA WA MOROGORO JANA.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Facebook Themes